pole pole, humprey pole pole, humprey

SIASA ZA ULAGHAI NA HUMPREY POLEPOLE.

Kiongozi au Mfitini?

Katika siku za karibuni, jina la Humphrey Polepole limezidi kusikika kwenye majukwaa ya siasa na mitandao ya kijamii. Si kwa mafanikio ya kisiasa au ujenzi wa hoja mpya za maendeleo, bali kwa malalamiko, shutuma na maneno makali dhidi ya serikali ya chama chake mwenyewe – Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hii ni sura halisi ya kile kinachoitwa siasa za ulaghai, ama Mfitini na hapa chini Ninaeleza kwa nini.

Kumbukumbu za Pole Pole wa kipindi cha Magufuli:

Nina Imani kuwa wote hatujasahau kuwa Polepole alikuwa miongoni mwa maafisa waandamizi walioaminika na Hayati Rais John Magufuli. Wakati huo, aliitumia kila fursa kutetea serikali  hata katika mazingira ambayo wananchi walikuwa wakilalamikia maamuzi yaliyokuwa yakiwadhuru, iwe ndani ama nje ya chama.

Katika kipindi hicho, Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais, hakuwahi kupewa uzito unaostahili, si kwa sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake, bali kwa sababu ya jinsia yake. Ushahidi wa dhuluma hii ya kimfumo unaonekana hata kwenye safu ya ulinzi wake, ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa ya wanaume, jambo lililozua maswali kuhusu heshima kwa viongozi wanawake.

Njama Baada ya Kifo cha Magufuli

Baada ya kifo cha Rais Magufuli, taarifa zisizo rasmi zinaeleza kuwa Polepole na baadhi ya viongozi waliokuwa karibu naye, walijaribu kutumia njia za ndani ya chama kuzuia kuapishwa kwa Rais Samia. Hii ni kwa sasabu walihofia kuongozwa na mwanamke, yule yule waliyekuwa wakimdharau hadharani kipindi ni makamu wa Rais. Ingawa juhudi hizo hazikufanikiwa, ila zilichelewesha kwa njia isiyoeleweka mchakato wa kumuapisha Samia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kashfa ya Bandari na Mradi wa Magari ya V8

Katika kipindi hicho hicho, akiwa kiongozi mkubwa wa CCm kuna tuhuma nzito zinazomhusu Polepole akihusishwa na mpango wa kifisadi bandarini  ambako magari aina ya Toyota V8 yaliagizwa kwa kivuli cha CCM, lakini yakaingizwa nchini bila kulipiwa ushuru. Baadaye magari hayo yaliuzwa kwa bei ya kutupwa, kwa maslahi yake na serikali ikakosa mapato. Huu ulikuwa ni wakati ule ule ambapo ulizuka msemo wake maarufu “Unaijua Vietee wewe?

Kashfa za Maadili Binafsi

Mbali na siasa, kuna tuhuma za kimaadili zinazomkabili Polepole. Zikimhusisha na mahusiano ya siri na wasaidizi wa kike wa vyuoni pamoja na wake za watu. Hadi sasa hajawahi kutambulika kwa ndoa wala kuwa na familia rasmi jambo ambalo linatia shaka kuhusu uimara wa misingi ya maadili kwa mtu anayejiweka kama mtetezi wa maadili ya kisiasa na kijamii.

Kutopata Anachotaka Siyo Sababu ya Kuchafua Serikali

Sio kwamba tunahalalisha kuwa hana mchango wowote katika chama wala nchi lakini Inashangaza kuona Polepole, aliyesomea Diplomasia na kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania, kuitumia nafasi hiyo kushambulia hadharani serikali ya nchi yake. Huu ni ulaghai kwa sababu aliwahi kutoa shutuma na ukosoaji kupitia kipindi chake alichokirusha kupitia channel ya Youtube Kipindi ambapo alitengwa na mfumo, lakini mara tu baada ya kupewa cheo cha ubalozi akaufyata, kwa wakati huo hakuona ukiukwaji wa aina yoyote ila kwa sasa ndio anajinasibu kuwa kuna mambo mbali mbali yanakiukwa.

Fununu zinaeleza kuwa kuna watia nia wa ubunge aliowapendekeza kwa maslahi yake binafsi ambao walikatwa mapema  hali iliyomvunja moyo na ukizingatia yupo mbali na siasa za Tanzania kwa hivyo ameendelea Kujawa na hofu dhidi ya maslahi yake kwenye chama, hivyo huenda ameamua kutumia trick ya kujiuzulu ili aweze kurudi katika siasa nchini.

Ndio maana tunamuita, mfitini mwenye Siasa za ulaghai kutokana na mbinu zake za kuwaadaa watanzania ili kuonekana kuwa ni mtu mwema, mpenda maendeleo wakati amehusika kwa namna nyingi kuminya maoni na haki za  watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *