Kwa sasa, tusikubali kutumika. Tuchambue fact. Tuilinde amani yetu. Siasa itapita, lakini taifa ni letu sote. Kwa sasa, tusikubali kutumika. Tuchambue fact. Tuilinde amani yetu. Siasa itapita, lakini taifa ni letu sote.

DRAMA ZA CHADEMA KATIKA MISINGI YA KISHERIA

Kwa sasa, tusikubali kutumika. Tuchambue fact. Tuilinde amani yetu. Siasa itapita, lakini taifa ni letu sote.

Katika siku ya jana, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilijikuta tena kwenye mvutano mkali na Jeshi la Polisi, kufuatia tukio lililotokea mahakamani ambapo kiongozi wao, Tundu Lissu, alikuwa anafikishwa. Taarifa zinaonesha kuwa kulikuwa na mkusanyiko wa watu waliodaiwa kuwa wafuasi wa chama hicho waliokusanyika katika eneo la mahakama, kinyume na onyo lililotolewa awali na Jeshi la Polisi.

Kabla ya tukio hilo, Polisi walitoa tamko wazi wakionya kwamba hali ya usalama ilikuwa tete, hasa kutokana na kauli kali za baadhi ya viongozi wa CHADEMA waliotishia “kumchukua” Lissu kutoka mahakamani, pamoja na miito yao kwa wananchi kujitokeza kwa wingi mahakamani. Katika mazingira hayo, ni wazi kwamba kulikuwa na tahadhari ya kiusalama, lakini onyo hilo lilikaidiwa na wafuasi wa chama hicho.

Kilichofuata baada ya hapo ni kile kinachotajwa na CHADEMA kama “kuvunjwa kwa raia”, wakionesha watu waliobebwa huku wakilia na kudai kuumizwa vibaya na polisi. Hata hivyo, ukitazama kwa karibu video na picha zilizotapakaa mitandaoni, ni vigumu kuamini kama kweli walivunjwa miguu. Wengi wanaonekana wakilalamika, wakibebwa na kuanguka hovyo hovyo, lakini hakuna dalili halisi zinazoonesha majeraha makubwa kama ya kuvunjika kwa viungo. Hili nalo linazua maswali mengi.

Kwa mtu ambaye amewahi kuvunjika mguu au kushuhudia mtu aliyevunjika, anaweza kuelewa tofauti ya maumivu halisi na maigizo. Kwa mtazamo wangu, kuna kila dalili kuwa baadhi ya haya matukio ni ya kupangwa ili kupandikiza chuki kwa Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla. Ni kama mbinu ya propaganda inayolenga kuchochea hisia na chuki kwa umma dhidi ya vyombo vya dola.

Swali la kujiuliza ni: Wanatumika kwa faida ya nani? Je, ni mkakati wa kisiasa wa kuonesha kuwa serikali ni dhalimu? Au ni njia ya kukusanya huruma ya umma kuelekea uchaguzi? Tunapaswa kutambua kuwa, mbinu hizi za kuchokoza polisi kisha kuja kulia mbele ya kamera, zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa ustawi wa nchi na zimepitwa na wakati.

Watanzania wengi kwa sasa wameelimika na wana uwezo wa kuchambua habari kwa kina. Hii ndiyo sababu ni muhimu sana sisi kama wananchi tunabidi kujifunza kuchuja taarifa, kutafuta ukweli, na kutanguliza maslahi ya amani ya taifa letu kuliko mihemko ya kisiasa.

Kwa sasa, tusikubali kutumika. Tuchambue fact. Tuilinde amani yetu. Siasa itapita, lakini taifa ni letu sote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *