Historia Imeandikwa Nane Nane! Historia Imeandikwa Nane Nane!

HISTORIA IMEANDIKWA NANE NANE 2024!

Kwa mara ya kwanza, Tanzania imeshuhudia mabadiliko makubwa katika kilele cha Maonyesho ya Kimataifa ya Nane Nane, Huku Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maabara Kuu ya Kilimo inayojengwa katika Mji wa Serikali, Dodoma, mradi ambao umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 16.

Mhe. Rais Samia pia alitembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho, ambapo alipata fursa ya kujionea bidhaa na teknolojia za kisasa zinazohusiana na kilimo. Aidha, alikabidhi tuzo kwa washindi waliobobea katika sekta ya kilimo, hatua inayolenga kutambua na kuhamasisha juhudi zao.

Mbali na hayo, Mhe. Rais aliendesha zoezi la makabidhiano ya zana za kilimo, ikiwemo matrekta 519, power tillers 800, na majembe ya kulimia 200. Zana hizi zitachochea mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa kilimo nchini.

Rais pia alimwagiza Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (MB), kuhakikisha ahadi ya kuwafikishia wakulima zana 10,000 inatimizwa ifikapo mwaka 2030.

Hatua hizi ni muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata nyenzo za kisasa zinazowawezesha kuongeza tija na kuboresha maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *