SIKU 100 ZA RAIS SAMIA SEKTA YA MADINI SIKU 100 ZA RAIS SAMIA SEKTA YA MADINI

SIKU 100 ZA RAIS SAMIA SEKTA YA MADINI. 

Katika siku mia moja za kwanza za kipindi cha pili cha uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa hakika Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kudhihirisha kwa vitendo dhamira yake ya kuimarisha misingi ya uchumi wa Taifa, kusimamia rasilimali za nchi kwa uwazi na kuhakikisha wananchi wananufaika moja kwa moja na utajiri wa Taifa lao. 

Sekta ya Madini imeibuka kama mojawapo ya sekta kinara zinazokua kwa kasi, yenye mwelekeo na matokeo chanya ya utekelezaji chini ya maelekezo ya Rais katika kipindi kifupi lakini chenye tija.

Kwa mfano, Kupitia Wizara ya Madini, ndani ya Siku 100 za mhe Rais, Wizara imeongeza mapato ya Serikali, na kukuza mchango wa sekta katika Pato la Taifa, vilevile imejidhatiti kuongeza thamani ya madini ndani ya nchi, kuimarisha ushiriki wa Watanzania pamoja na kusimamia rasilimali za madini kwa misingi ya haki, uwazi na uwajibikaji.

Mapato ya Madini: Takwimu za Mafanikio.

Moja ya mafanikio makubwa yaliyojitokeza katika siku 100 ni ongezeko la makusanyo ya maduhuli yatokanayo na sekta ya madini. Kabla ya marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017, sekta hii ilikuwa ikichangia mapato kidogo ukilinganisha na ukubwa wa rasilimali zilizopo. Hata hivyo, maboresho ya kisheria na kiutawala yameleta mageuzi makubwa.

Katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, Wizara ya Madini iliwekewa lengo la kukusanya Shilingi Tsh trillion 2.1 . Kufikia Desemba 2025,  Mpaka kufikia tarehe 25-1-2026 sekta ya madini imekusanya zaidi ya billion 741 sawa sawa na Asilimia 62 ya makusanyo yote yanayohitajika Kwa Mwaka mzima. Mafanikio haya yametokana na uimarishaji wa mifumo ya usimamizi wa leseni, udhibiti wa biashara ya madini, ufuatiliaji wa uzalishaji pamoja na mapambano dhidi ya utoroshaji wa madini.

Siku 100 za kwanza za Mhe Rais Kwa sekta ya madini.

Katika kipindi cha siku 100, mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umeendelea kuongezeka kwa kasi. Kama mnakumbuka Mwaka 2024, sekta ilichangia asilimia 10.1 ya Pato la Taifa, ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2020. Mwelekeo huu umeimarika zaidi katika mwaka 2025 ambapo mchango ulifikia asilimia 11 katika robo ya kwanza na kuongezeka hadi asilimia 12 katika robo ya pili.

Takwimu hizi zinaonesha wazi kuwa Sekta ya Madini sasa imekua sekta kuu, na mhimili muhimu wa uchumi wa Taifa, ikienenda sambamba na dira ya Rais Samia ya kuijenga Tanzania yenye uchumi shindani na jumuishi.

Harakati za Uongezaji Thamani Madini

Katika utekelezaji wa ahadi ya kuongeza thamani ya madini, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha Mkakati wa Uongezaji Thamani Madini wa miaka mitano (2026/27–2030/31). Mkakati huu umetambua mikoa sita ya kimadini—Arusha, Dodoma, Kahama, Mbeya, Lindi na Pwani—kama vituo vya awali vya viwanda vya uongezaji thamani.

Kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Serikali pia imeimarisha uwepo wa viwanda vya kusafisha na kuongeza thamani madini. Hadi sasa, Tanzania ina refinery sita za dhahabu, smelter mbili za tin, smelter 13 za shaba, smelter tatu za nikeli na smelter nne za graphite. Hatua hizi zimepunguza uhamishaji wa thamani nje ya nchi, zimeongeza ajira na zimechochea ukuaji wa viwanda vya ndani.

Sambamba na hilo, tumejipambanua katika ujenzi wa Kituo cha Jemolojia Tanzania jijini Arusha chenye thamani ya Shilingi bilioni 33 umeanza na kufikia asilimia 10. Mradi huu unatarajiwa kuifanya Arusha kuwa Kituo cha Madini ya Vito barani Afrika.

Leseni, Masoko na Urasimishaji wa Wachimbaji Wadogo

Katika siku 100, Wizara ya Madini tayari imeratibu utoaji wa leseni 12,130 sawa na asilimia 117.8 ya lengo la mwaka. Aidha, kati ya Julai hadi Desemba 2025, leseni 7,523 zilitolewa, sawa na asilimia 146 ya lengo la kipindi husika. Hatua hii imeongeza uwekezaji, ajira na urasimishaji wa shughuli za wachimbaji wadogo.

Biashara ya madini yenye thamani ya Shilingi trilioni 3.102 imefanyika katika masoko 44 na vituo vya ununuzi 117 nchini, jambo lililowapa wachimbaji soko la uhakika na bei shindani.

Watanzania Kuwekwa Katikati ya Uchumi wa Madini

Ukiachana na mafanikio yote hayo, serikali bado inawakumbuka wananchi, na kupitia Utekelezaji wa sera ya Local Content umeleta mapinduzi makubwa katika ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya madini. 

Mwaka 2024, jumla ya manunuzi ya migodi yalifikia takribani Shilingi trilioni 5, ambapo Shilingi trilioni 4.41 (asilimia 88) zilitoka kwa makampuni ya Kitanzania. Huu ni ukuaji kutoka asilimia 61 hadi 88 ndani ya miaka sita pekee, ishara tosha ya utekelezaji madhubuti wa maelekezo ya Rais Samia.

Utafiti wa Jiolojia na Teknolojia ya Kisasa

Katika siku 100, sampuli zaidi ya 19,700 zimechambuliwa na utafiti wa jiolojia katika maeneo ya Kibiti na Rufiji uliongeza eneo lililofanyiwa utafiti hadi asilimia 98. Serikali pia imekamilisha usimikaji wa vituo 32 vya kufuatilia mitetemo ya ardhi, hatua inayoongeza usalama na uendelevu wa shughuli za madini.

Madini na Ajenda ya Nishati Safi

Kupitia STAMICO, Serikali imeanza utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia Rafiki Briquettes. Mitambo miwili ya uzalishaji inasimikwa Tabora na Dodoma, huku taasisi za elimu, afya, masoko na vyombo vya ulinzi vikianza kutumia nishati hii rafiki kwa mazingira.

Mining for a Brighter Tomorrow (MBT): Madini kwa Maendeleo Jumuishi

Kama hujui pia, serikali imeanzisha Programu maalumu ya MBT ambayo imeanzishwa mahsusi kuwajumuisha vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum katika mnyororo wa thamani wa madini. Hatua ambayo inaakisi falsafa ya Rais Samia ya maendeleo jumuishi yasiyomwacha mtu nyuma.

Hitimisho

Kwa ujumla, siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha pili cha uongozi wake zimeonesha kwa vitendo kuwa Sekta ya Madini iko kwenye njia sahihi ya kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa. Kupitia uongozi thabiti, sera makini na utekelezaji wenye matokeo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *