Tanzania na Mageuzi mapya ya Kiuchumi na Kidiplomasia: kutoka Hotuba ya Kihistoria ya Diplomasia 2026 Tanzania na Mageuzi mapya ya Kiuchumi na Kidiplomasia: kutoka Hotuba ya Kihistoria ya Diplomasia 2026

TANZANIA NA MAGEUZI MAPYA YA KIUCHUMI NA KIDIPLOMASIA

Na Mwandishi wetu

Hotuba ya siku ya jana iliyotolewa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Kidiplomasia uliofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma,naweza kusema kuwa ni moja ya hotuba zenye uzito mkubwa kisera, kiuchumi na kidiplomasia katika historia ya Tanzania.

Kama ulitega vyema sikio lako ni hakika haikuwa ya kimzaha bali ilitoa tamko la mwelekeo mpya wa taifa katika dunia tuliyopo yenye misukosuko ya kiusalama, kiuchumi na kimazingira. Katika mazingira ya dunia ya sasa ambapo migogoro ya kivita inaendelea (Ulaya Mashariki, Mashariki ya Kati), uchumi wa dunia unakabiliwa na mdororo wa ukuaji, minyororo ya mauzo imevurugika, na mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuathiri uzalishaji, Tanzania inajitokeza kwa kipindi hiki kama mfano wa uthabiti wa kisera na uthamini wa diplomasia kama nyenzo ya maendeleo.

Uchumi wa Tanzania Katika Muktadha wa Dunia (2025) Kwa mujibu wa takwimu kutoka hotuba ya mhe Rais imetoa picha ya uchumi imara kwa viwango vya nchi zinazoendelea. Katika hotuba yake ameeleza kuwa uchumi umeendelea kukua kwa karibu asilimia 6 ya Pato la Taifa (GDP) ambao umeendelea kuiweka Tanzania juu ya wastani wa ukuaji wa dunia uliokadiriwa kuwa chini ya asilimia 3 mwaka 2025.

Aidha, kiwango cha mfumuko wa bei cha asilimia 3.3 ni bora zaidi ikilinganishwa na nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo baadhi zimeshuhudia mfumuko wa zaidi ya asilimia 10 kutokana na misukosuko ya bei ya nishati na chakula. Sambamba na hilo, pia tunaona Uwiano wa deni la taifa kusalia asilimia 48.2 ambapo tunaweza kusema kuwa bado ni chini ya kikomo cha hatari cha asilimia 55 kwa nchi zenye kipato cha chini.

Hali inayoiweka Tanzania katika nafasi nzuri ikilinganishwa na mataifa kama Kenya au Zambia ambayo katika miaka ya karibuni yamekumbwa na migogoro ya madeni. Hili linaakisi nidhamu ya kifedha na usimamizi makini wa uchumi.

Uaminifu wa Wawekezaji na Rekodi ya Miradi Kwa mujibu wa takwimu tumeshuhudia Mwaka 2025 ukiweka historia mpya katika uwekezaji. Hii ni baada ya Usajili wa miradi 927 yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 11.4 za Marekani ambayo ishara ya wazi ya kuimarika kwa imani ya wawekezaji.

Hili ni ongezeko la asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia na hii inaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa masoko yanayovutia zaidi Afrika Mashariki, sambamba na Kenya na Ethiopia. Cha kuvutia zaidi katika suala la uwekezaji ni ushiriki wa wawekezaji wa ndani (asilimia 31 ya miradi), jambo linaloashiria kukua kwa biashara na ujasiliamali kwa Watanzania, tofauti na nchi nyingi zinazoendelea ambazo bado zinategemea zaidi mitaji ya nje.

Katika uwekezaji huu tunategemea kama wananchi kunufaika na Ajira zaidi ya 162,000 zinazotarajiwa kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana. Mapinduzi ya Sekta Muhimu za Uchumi Katika sekta ya kilimo, kama nchi tumeendelea kujitosheleza chakula kwa kiwango cha asilimia 120 ambacho kunaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya usalama wa chakula, ukilinganisha na baadhi ya nchi kama Burundi ambayo ina GHI score ya alarming kukubwa na njaa kutokana na ukosefu wa ardhi, mvua zisizo za kawaida, na changamoto za kiuchumi.

Vilevile nchi kama Kenya ambayo imeelezwa kuwa Takriban milioni 1.8–3+ inakabiliwa na viwango vya juu vya njaa (IPC Phase 3+), hasa maeneo ya kaskazini na mashariki kutokana na ukame na mvua duni ya 2025. Katika Sekta ya madini imeeendelea kuoensha kasi ya kipekee katika ukuaji baada ya ongezeko la uzalishaji la zaidi ya asilimia 48, ikiongozwa na dhahabu, makaa ya mawe na madini ya ujenzi.

Vilevile serikali imeweka Mkakati mzuri sana wa kuhitaji angalau asilimia 20 ya dhahabu inayosafishwa kuuzwa Benki Kuu ili kuimarisha upatikanaji wa fedha za kigeni nchini. Utalii nao umeendelea kuwa injini muhimu ya mapato ya fedha za kigeni, ukiwa umefikia dola bilioni 4 mwaka 2025.

Hii imeifanya Tanzania kupokea tuzo kama Kituo Bora cha Safari Duniani 2025 ambazo zinaongeza hadhi ya nchi yetu kimataifa. Miundombinu, Viwanda na Ushindani wa Kikanda Kwenye suala la miundombinu serikali ya awamu ya sita imejipanga pia, ambapo tumeshuhudia Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), kukamilika kwa Bwawa la Julius Nyerere, na utekelezaji wa bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) ambayo inakwenda kuwa nguzo kubwa ya uchumi wa uzalishaji.

Miradi hii inaifanya Tanzania kuwa lango la biashara kwa nchi zisizo na bandari. Vijana nao hawajaachwa nyumba, tumeona serikali imechukua hatua za Kuanzisha Wizara ya Vijana chini ya Ofisi ya Rais hatua ambayo ni ya kimkakati baada ya kutambua wingi wa vijana na kero za vijana zinahitaji mamlaka husika kwa ajili ya kutafuta suluhisho na kuwawezesha.

Kwa ujumla, hotuba ya jana ya mhe rais imegusa kila idara, ikionesha mwanga na ramani ya safari ya Tanzania katika kipindi kijacho na imetuonesha uchu wa serikali kujifunza kutokana na makosa, changamoto ili kusonga mbele pamoja tukiwa wamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *