Kwa watu walio wengi, Umoja wa Ulaya (EU) unaonekana kwa sura ya nje kama chombo cha ushirikiano wa mataifa ya Ulaya kwa lengo la kuimarisha amani, biashara na maendeleo. Hata hivyo, wakosoaji wameibuka na kudai kuwa mfumo wa uongozi wa EU hauko wazi kabisa kwa wananchi, na kwamba maamuzi mengi hufanywa na baadhi ya watu ambao pia hawajachaguliwa moja kwa moja na wananchi.
Usichokijua kuwa katika EU, mamlaka makubwa yapo chini ya Tume ya Ulaya (European Commission). Na wajumbe wakuu wa tume hii, wanaojulikana kama makamishna, huteuliwa na serikali za nchi wanachama kwa siri na sio kupigiwa kura na wananchi. Hii imekuwa ikizua hoja kwa mataifa makubwa ikiwemo Marekani kwamba watu walio madarakani (EU) Brussels hawana uwajibikaji wa moja kwa moja kwa wananchi wa kawaida.

Kinachozidi kuzua mjadala na hofu zaidi ni kwamba Tume ya Ulaya imejipatia nguvu kubwa ya kupendekeza sheria, kusimamia utekelezaji wake, na kuhakikisha bidhaa na sera za pamoja zinafuatwa. Hata Bunge la Ulaya, ambalo wanachama ama wawakilishi wake huchaguliwa na wananchi, halina nguvu za mwisho za kuzuia au kufuta maamuzi yote ya tume hiyo kwa urahisi. Na kwa ufupi hawana uvumilivu kwa wakosoaji ama mataifa ambayo hayaendani na matakwa yao.
Mfano unaotajwa mara kwa mara ni kiongozi wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ambaye alipata nafasi hiyo kupitia kuwashawishi kwa njia za siri wanasiasa wa ndani ya vyama vikuu barani Ulaya. Wapo waliodai hakukuwa na uwazi wa kutosha katika mchakato huo.

Pia, EU imekuwa ikikosoa na kuchukua hatua dhidi ya nchi kama Hungary na Poland kwa madai ya kukiuka misingi ya demokrasia na utawala wa sheria. EU imezuia au kuchelewesha fedha kwa nchi hizo, hali ambayo wakosoaji wanaiona kama mbinu ya kushinikiza nchi zikubali sera fulani, ikiwemo masuala ya wahamiaji na mageuzi ya mifumo ya mahakama.
Umati wa wa marekani pia wamekuwa na wasiwasi kuhusu sheria za EU mpya za udhibiti wa maudhui mtandaoni, kama ilivyopamba moto katika mtandao wa X, wakidai zinaweza kutumika kupunguza uhuru wa maoni chini ya kisingizio cha kupambana na habari za uongo na chuki.

Kwa ujumla, mjadala mkubwa unaoendelea ni je, EU ni chombo cha ushirikiano wa hiari kati ya mataifa huru, au ni mfumo tu,, uliojikusanyia mamlaka mengi mikononi mwake kwa ajili ya kushurutisha taasisi na mataifa yaliyochaguliwa moja kwa moja na wananchi? Majibu ya swali hili yanategemea upande wa mtu katika siasa