SAMIA AZINDUA SGR SAMIA AZINDUA SGR

UZINDUZI WA TRENI YA SGR UNAKUJA NA MAPINZDUZI MAKUBWA NCHINI.

Leo, watanzania tunajivunja kuzindua rasmi sehemu ya kwanza ya reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Mradi huu tuliousubiri kwa hamu ni hatua muhimu katika mabadiliko ya miundombinu ya usafiri nchini, ukiwa na uwezo wa kubadilisha uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.

Reli ya SGR, inayoanzia Dar es SALAAM, Morogoro na hadi Dodoma, imejengwa kwa teknolojia ya kisasa, ikiwa na uwezo wa kusafirisha abiria na mizigo kwa kasi zaidi na gharama nafuu. Hii inasaidia kupunguza muda wa safari na kuleta urahisi katika usafiri wa watu na bidhaa nchini.

Treni hiii ya umeme kama ilivyokuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ni kuunganisha sehemu mbalimbali za nchi na hadi kuunganisha nchi jirani, hivyo hii itaifanya nchi yetu Tanzania kuwa katika nafasi nzuri ya kukua kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki
Faida za Kiuchumi na Kijamii kupitia Reli ya SGR:


Mradi wa SGR umezalisha ajira kwa maelfu ya Watanzania, ukichochea ukuaji wa Uchumi kwa maeneo inapopita. Pia, unatarajiwa kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo, hivyo kufungua milango zaidi kwa biashara za ndani na nje ya nchi. Mfumo huu wa reli utaimarisha uwekezaji wa kigeni na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine kama vile utalii na viwanda.

SGR imejengwa kwa kuzingatia viwango vya juu vya usalama na teknolojia ya kisasa, ikiwa na mifumo ya usalama inayoendana sawa na ile inayotumiwa katika nchi zilizoendelea.

Hii inachochea amani na usafiri ulio salama na wa kuaminika kwa abiria na mizigo, na hivyo kuboresha huduma za usafiri nchini na bila shaka kupunguza matukio ya kiuhalifu na yasiyo ya kiusalama kama vile ajali na za magari, wizi nk ambayo yamekuwa kero kwa muda mrefu hapa nchini kwa usafiri wa nchi kavu.

Uzinduzi wa SGR ni ushahidi wa dhamira ya Rais Samia na serikali yake katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii kupitia miundombinu bora. Ni hatua inayodhihirisha uwezo wa Tanzania katika kuboresha maisha ya watu wake na kuweka misingi ya maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo.

Ni wajibu wetu sasa Watanzania kutunza miundombinu hii ya Reli ya SGR, ili kuhakikisha rasilimali hizi zinadumu kwa muda mrefu na kuendelea kuisadia Serikali na mapambano dhidi ya umasikini.

Dkt Samia Suluhu Hassan kusimamia kukamilishwa kwa utekelezaji wa mradi huu utaingia daima kwenye historia ya maendeleo ya nchi yetu Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *