TUIBUE WATANZANIA WENYE VIPAJI NA UBUNIFU KATIKA TEKNOLOJIA.


Rais Samia Suluhu Hassan Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia mwaka 2024 jijini Dar es Salaam, ametoa wito kwa Wizara ya Nishati nchini Tanzania kutafuta Watanzania wenye vipaji na ubunifu katika teknolojia, ili waweze kusaidia katika kutekeleza mpango wa kutoa huduma ya gesi ya kupikia kwa mfumo unaofanana na ule wa LUKU za umeme.

Rais Samia amesisitiza umuhimu wa serikali kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuweka sera bora zitakazosaidia kufikia malengo ya mkakati huo.


Aidha, Rais Samia amezitaka sekta binafsi kuchangia katika juhudi za kuongeza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa kuboresha miundombinu na kuwekeza zaidi.

Pia, amewataka kuleta teknolojia rahisi zitakayowezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na mfumo wa kulipia kadri wanavyotumia, kama ilivyo kwa umeme na maji kwa kutumia mita za malipo kabla ya matumizi.

Rais Samia ameongeza kuwa ameshuhudia teknolojia hiyo katika maonyesho ya mazingira yaliyowahi kufanyika huko nyuma, ambapo Watanzania walifanikiwa kutengeneza mitungi ya gesi ambayo inaruhusu watumiaji kulipia gesi wanayotumia kulingana na mahitaji yao.

Hivyo, ameitaka Wizara ya Nishati kuwatafuta au kuwahimiza Watanzania wenye uwezo huo ili waweze kushirikiana katika kuleta mabadiliko katika sekta hiyo.


Vile vile, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa agizo kwamba matumizi ya gesi sasa ni lazima na siyo anasa tena.

Mhe Rais amesema hayo akimuelekeza Waziri Mkuu na Wizara ya nishati kuhakikisha wanaweka katazo ambalo ifikapo Agosti mwaka huu, taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100 zipige marufuku matumizi ya kuni na
mkaa.

Rais Samia pia amesisitiza kuwa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo itapaswa kuwasilishwa ndani ya miezi mitatu ijayo. Amezungumzia kwamba majaribio ya awali yameonyesha mafanikio, hivyo sasa ni wakati wa kuweka katazo rasmi.

Mhe Rais anasistiza kwamba matumizi ya nishati safi ya kupikia sasa ni hitaji la lazima, akisisitiza kuwa gesi si hatari kama ilivyokuwa ikifikiriwa hapo awali.

Aidha, Rais Samia amewataka mama lishe kuhamasishwa kutumia gesi badala ya kuni na mkaa na kwa wale wanaokuja kuomba huduma za kupikia, waelezwe kuhusu faida za kutumia gesi, na kwamba juhudi zitafanyika ili wapewe mafunzo ya namna ya kutumia
gesi vizuri.

Kama umetega sikio lako vema kumsikiliza Mhe Rais utagundua kuna
mwamko na msisitizo mkubwa wa katika matumizi ya nishati safi ambayo yanaonesha jitihada za serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Agizo la kufanya matumizi ya gesi kuwa lazima katika taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100 ni hatua muhimu kuelekea kufikia malengo ya mkakati wa nishati safi ya kupikia.

Hatua itasaidia siyo tu katika kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ambayo
yanachangia uharibifu wa mazingira na afya ya binadamu, lakini pia inaimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa wananchi.

Katika kuhamasisha matumizi ya gesi, serikali itasaidia kuboresha afya za watanzania na mazingira safi kwa kuepusha uchafuzi wa hewa unaosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Katika kuhamasisha matumizi ya gesi, serikali itasaidia kuboresha afya za watanzania na mazingira safi kwa kuepusha uchafuzi wa hewa unaosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Pia, itatoa fursa za kiuchumi kwa kukuza soko la gesi na kuchochea uvumbuzi katika teknolojia za nishati safi.

Rais anasistiza zaidi kuwa “Hatuwezi kupoteza Nguvu Kazi ya Taifa, Hasa Wanawake kwasababu Matumizi ya Nishati isio Safi”

Kwa mujibu wa ripoti zinaonesha kuwa zaidi ya 90% ya kaya za Tanzania zinategemea matumizi ya nishati isiyo safi mfano Mkaa, Kuni, Vinyesi vya wanyama kwa matumizi ya nyumbani.

Kati ya vipaumbele vya Mhe. Rais Dkt. Samia ni kuhakikisha Tanzania inaweka mikakati sahihi kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuchochea matumizi ya nishati safi.

Hivyo basi, Serikali ya Awamu ya Sita, kupitia Wizara ya Nishati imezindua Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 lengo ni kuhakikisha 80% ya WaTanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2033

Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia itasaidia kupunguza ukataji miti kiholela kwa kupunnguza matumizi ya Nishati inayotegemea Misitu.

Mhe. Rais anaendelea kupigania haki na maisha bora kwa wanawake ambao wanaathirika zaidi kutokana na matumizi ya nishati isiyo rafiki.

Hili linathibitishwa na juhudi zake kama kuongoza mkakati wa nchi za Afrika kuwawezesha wanawake kutumia nishati safi katika mkutano wa COP28.

Jambo la mwisho la kutia moyo ni kuona serikali inazingatia mahitaji na uwezo wa kiuchumi wa wananchi katika mchakato huu ili kuhakikisha kwamba mfumo wa nishati safi unapatikana kwa bei nafuu na unapatikana kwa urahisi kwa kila mwananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *