NATAKA NIANZE kwa kusema suala la tatizo la sukari Tanzania halitakaa liishe kama tutaendelea kuwaacha ma cartel wa sukari wakiongozwa na mmiliki wakiwanda cha sukari cha Kagera Sugar (mmiliki wa Super Doll) bwana Seif Ali Seif na watu walioko ndani ya bodi ya sukari Tanzania.
Luhanga Mpina huwezikuwa mtu sahihi wa kusema haya mambo kwa kuwa wewe una interest na familia ya Seif Ali Seif awa Super Doll na tunajua jinsi ambavyo ulishirikiana nao ukiwa waziri wa mifugo na uvuvi kupewa zaidi ya pande la ardhi la heka 20,000 huko Kagera na tunajua una maelfu ya ng’ombe ndani ya ranch yao huko Kagera na mmejimilikisha mapande ya ardhi maeflu ya hekari mlizompora yule mwekezaji wa kizungu kwa kigezo kuwa hana mtaji wa kuendeleza eneo hilo.
Mpina wewe ni CANCER ndani ya taifa hili kwa sababu kuna uchafu mwingi sana umefanya ukiwa na Seif Ali Seif mkisaidiwa na Magufuli mlipokuwa mnagombania mashamba na ranchi huko Kagera. Mbona huwaambii watanzania kuwa Seif Ali Seif alimpa Magufuli ranchi ya hekari 200,000 huko Kagera? Mbona husemi mlimpora mwekezaji wa kizungu hekari 60,000 mkazimiliki wewe na Super Doll?
SUALA la sukari Tanzania tunajua linaendeshwa na ma cartel na majizi yakiongozwa na Seif Ali Seif ambao kwa sababu za kijambazi tu walitaka bei ya sukari ipande kwa shilingi 1000/= permanently na hawakutaka ipungue hata kama uhaba umepungua na yote hii inafanywa na kundi hili ili kupata faida kubwa sana.
Kundi hili ndilo liko nyumna ya Mpina baada ya kufeli kutumia vyombo vya habari kusambaza mambo haya mbali na kuwaahidi kuwalipa 30m TZS kila gazeti litakaloandika habari hii ndiyo maana sasa wamegeukia akina Mpina na kutumia social media kusambaza ajenda yao hii.
SWALI nalojiuliza tunapokuwa na crisis kama ya sukari na watu wanataka sukari cha kwanza tunaangalia nani analeta sukari kusaidia watanzania au tunaangalia sifa za kampuni? Yaani hata kama ingekuwa ni kampubi ya kuuza mandazi ina uwezo wa kuleta sukari kwani kuna shida gani ikaleta sukari kama ina uwezo na ikakidhi shida kwa wakati huo?
Kama serikali mlitaka ifanyeje wakati kikundi cha watu wachache wawakoseshe sukari watanzania milioni 60 kwa kuwa tu kikundi cha ma cartel kimeamua kukataa kuagiza sukari na kuficha sukari? Hakuna serikali duniani ya kijinga hivyo inayoweza kukubali wafanyabiashara wa aina ya Super Doll waitie nchi kwenye crisis kwa kuwa tu wameamua kutengeneza shida.
Hivi kweli Super Doll na nyie watu wa bodi ya sukari kwa akili zenu kabisa mnataka kuongeza bei ya sukari kwa shilingi 1000/= kwa kilo permanently bila kujali kuwa uhaba au hakuna. Kama wakati wa uhaba bei inapanda tunaelewa kwa sababu hayo ni mambo ya kiuchumi lakini yaani sukari ipo na inazalishwa kwa wingi halafu bado mnataka ongezeko la 1000/= kwa kilo liwe la kudumu? Hivi nyie mko sawa kweli? Mnawaonaje watanzania?
Tunajua kuwa Mpina anashikirikiana na Super Doll na wanahonga baadhi ya wabunge shilingi 30m TZS kila mmoja kwa lengo la kupinga hoja na sheria ya kutaka NRFA ipewe uwezo wa kisheria kununua sukari na kuisambaza nchini.
Swali ni kwa nini Super Doll na kundi la majizi menzake wanatumia fedha nyingi kiasi hiki kukwamisha suala hili? Kama wao hawahusiki na uharamu wa usambazaji wa sukari nchini wanawezaje kulipa zaidi ya wabunge 25 shilingi 30m kila mmoja kupinga suala hili?
Watanzania tunawaambia haya ili muwe makini mkiona kila mbunge anasimama na kupinga kuanzishwa kwa sheria ya kutaka NRFA kununua na kusambaza sukari basi kaeni mkijua ni miongozi mwa waliowekwa mfukoni na Super Doll na kiranja wao ni Mpina.
Yaani serikali inapotafuta njia ya kudumu ya kushughulika na ma cartel haya ya sukari na majizi yanayotengeneza crisis ya sukari ili yapate faida sana na kuumiza watanzania kuna wabunge muda huu wameshalipwa na wanajiandaa kupinga kupitishwa kwa sheria hii.
Kwa maneno rahisi ni kuwa wanataka kundi la akina Seif Ali Seif wamendelee kuwashikilia mateka watanzania milioni 60 linapokuja suala la uhaba wa sukari kwa kuwa wao wanapata faida sana na hawajali lolote.
Yaani wabunge wa ajabu sana hawa. Mnawezaje kupinga muswada huu kwa manufaa ya watu wachache na kuizuia serikali kununua sukari na kuisabambaza kunapotokea upungufu nchini? Au na nyie mnafurahi wananchi wanapokuwa wanahangaika na ukosefu wa sukari? Au 35m mlizopewa kwenu ni kitu cha maana sana na mnasaliti wapige kura wenu? Mnasaliti watanzania? Mnasaliti chama chenu? Na zaidi ya yote mnamsaliti Rais wetu? Haiingii akilini kama kweli mbunge kachaguliwa kuwatetea watanzania leo anashirikiana na wahuni kama Mpina kukwamisha jambo kubwa na la maana sana linalokwenda kutibu uhuni unaofanywa na makampuni ya sukari yanayotengeneza crisis kila siku na kuongeza bei ya sukari kwa faida yao na kuumiza watanzania.
TUNAWAASA wabunge wa bunge la Tanzania kuwa makini sana na kuwasaidia watanzania kwenye shida hii kwa kupitisha hii sheria ya kuruhusu NRFA kupewa mamlaka ya kisheria ya kununua na kusambaza sukari ili suala hili lihamie mikononi mwa serikali kwa kuwa haya majizi ya akina Super Doll yanahangaika sana kukwamisha jambo hili kwa lengo la kuendelea kuwanyonya watanzania.
Mpina na kundi lake wao ni mawakala wa majizi haya ndani ya bunge la Tanzania na lengo lao ni kukwamisha muswada huu na kuona suala la sukari linaendelea kuwa ni tatizo sugu mikan endo miaka rudi. Haiwezekani lazima ifike mahali jambo hili lipate tiba ya kudumu na muda wake ni sasa.
CCM tunawatazama kwa makini sana na tunawashangaa sana mnapokuwa na Mbunge kama Mpina ambaye amegeuka kuwa mpinzani wa kila kitu ndani ya bunge na serikali ya chama chake kwa manufaa ya watu majizi kama akina Super Doll. Tunajua mtamshughulikia tu mwakani lakini kati ya sasa na mwakani anachofanya ni hatari sana kwa ustawi wa chama chake nan chi hii.