Tanzania imejulikana kama nchi yenye amani tangu ilipopata uhuru, na haijawahi kukumbwa na machafuko makubwa ya kitaifa. Ingawa kumekuwa na matukio madogo ya machafuko, serikali ya Tanzania imekuwa ikidhibiti kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha amani na usalama vinaendelea kudumu kwa wananchi wake.
Licha ya juhudi hizi, kuna changamoto zinazoibuka, ambazo hazizungumzwi sana, ikiwa ni pamoja na wale wanaojiita wanaharakati, ambao, badala ya kusaidia, wanachochea migongano na vurugu katika jamii. Mmoja wao ni Maria Sarungi, anayejulikana pia kama Shangazi.
Maria amekuwa akitumia misaada ya kifedha kutoka kwa mashirika makubwa mfano ni Ford Foundation kuendesha miradi ambayo inalenga kuvuruga amani badala ya kusaidia jamii. Kwa mfano, kupitia mradi wake wa Mwanzo Dot Org, kupitia channel yake ya Mwanzo TV ukipata kiasa cha dola za kimarekani 200,000 sawa na zaidi ya nusu bilioni, ukipata nafasi hata wewe unaweza kupitia tovuti ya Ford Foundation kupata taarifa hizi.
Maria ameonekana kubadili malengo ya misaada anayopokea kwa kuchochea vurugu na sintofahamu katika jamii, kama ilivyoonekana kwenye maandamano ya Wamaasai huko Ngorongoro, ambayo inadaiwa kufadhiliwa naye.
Maria si mtu wa kwanza wala pekee anayepokea msaada kutoka kwa Ford Foundation. Mashirika mengine nchini Tanzania yamekuwa yakinufaika na msaada huo na kufanya kazi ya kusaidia jamii kwa kweli, bila kuchochea migogoro.
Lengo la misaada hii kutoka Ford Foundation ni kuongeza uhuru wa kujieleza na kudai uwajibikaji, wanajulikana kwa hilo hata tukiangalia kwa majirani zetu Kenya, Lakini swali ni kwamba, Mbona wanaopata pesa hizo kutoka kwa Ford Foundation wanatumia lugha za staha na bila kuchochea uvunjifu wa amani, tusiende mbali, tuwatazame Jamii Forums wanadai uwajibikaji kwa lugha zenye staha bila kuchochea.
Lengo la mradi wa Maria lilionekana kuwa ni kutengeneza makala zinazodai kutetea haki za wanawake Afrika Mashariki, lakini, je, umewahi kuona makala yoyote inayotetea haki za wanawake kutoka kwake? Ni ipi nia yake? Ana kitu gani nyuma ya pazia? Imefikia hatua ya kuwaandikia wamasai mabango. Maandamano ya Wamasai yamefadhiliwa na nani?
Wamasai wanalalamikia kuwa hawana huduma nzuri za kijamii, jambo ambalo si la ukweli. Serikali imekuwa ikiwapatia huduma zote muhimu kama ilivyo kwa wananchi wengine. Kwa wale waliohamishwa, walikubali wenyewe kuondoka, wakijua kuwa watawekwa kwenye mazingira bora zaidi, na kutambua kuwa matumizi yao ya njia za kisasa yanaharibu ekolojia ya eneo hilo, ambalo ni urithi wa taifa na dunia. Kwa mfano, mwaka 2022, kaya 86 za Wamaasai zenye watu 453 ziliandikishwa kuondoka Ngorongoro kwa hiari.
Serikali imechukua hatua kadhaa kuhakikisha wale waliohamishwa wanapata huduma bora katika eneo jipya, ikiwemo kupima viwanja, kujenga nyumba, kutenga maeneo ya malisho, na kuweka miundombinu ya maji na umeme. Waziri Mkuu alieleza kuwa eneo la Handeni, Tanga, limetengwa kwa ajili ya makazi yao, likiwa na viwanja vya makazi, shule, zahanati, na huduma nyingine muhimu. Je, haya ndio wanayoyaita manyanyaso?
Pamoja na huduma hizi zote, kama taifa tunapaswa kufuata sheria. Kisheria, Rais ana mamlaka ya kuhawilisha ardhi kwa ajili ya manufaa ya umma, kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya Uhawilishaji wa Ardhi. Ni muhimu kwetu kuelewa sheria zetu kabla ya kutoa madai yasiyo na msingi.
Kupitia sheria ya Ardhi ya Kijiji, matumizi ya ardhi yanaweza kubadilika kuendana na mahitaji ya ardhi, ni wazi ongezeko la watu na ukuaji wa teknolojia haviwezi kukaa sehemu moja na sehemu ambayo inaitwa hifadhi ya taifa, itambulike kuwa kisheria hatua za uhawilishaji zilifuatwa. Kisheria pia mwananchi yoyote anayeishi katika ardhi inayofanyiwa uhawilishaji kwa matumizi ya hifadhi anastahili kulipwa fidia, na hicho ndicho kilichofanyika
Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba Maria anaishi Kenya, ingawa anapokea misaada kama Mtanzania. Hakuna kizuizi kutoka kwa serikali kinachomzuia kurejea Tanzania, lakini bado anatumia pesa alizopewa kuendesha Mwanzo TV, kueneza habari zinazochochea ghasia miongoni mwa Watanzania.
Maria ametumia njia ya kuchezea hisia za wananchi, na siku zote hisia huja mbele zaidi ya ukweli, jiulizeni kwanini serikali iwatoe wamasai? Wananufaika na nini? Je maamuzi uhawilishaji wa ardhi ya ngorongoro uliwekwa wazi? Kabla ya kutoa tuhuma kama mwananchi unawajibu wa kuutafuta ukweli.
Watu kama hawa wanahitaji kuchunguzwa kwa makini kwani wanatumika na nguvu za nje kuchochea vurugu kwa kivuli cha uanaharakati. Amani ni mali yetu sote, na ikiwa hatutaitunza, siku moja tutaijutia.